Vigezo 10 vinavyoangaliwa zaidi na wanaume kwa wanawake wanapotaka kuoa

0
58

Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba hukurupuka na kuoa mwanamke yeyote, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wataishi pamoja kwa kipindi chote cha maisha.

Kulingana na Wanasosholojia Christine B. Whelan kutoka Chuo Kikuu cha Pittsburgh, na Christie F. Boxer kutoka Chuo Kikuu cha Lowa wanabainisha vigezo vinavyoangaliwa zaidi na wanaume ili kupata wenza wao watarajiwa.

10: Mwenye uchu wa maendeleo

Licha ya dhana iliyoenea kwamba wanaume wanatishwa na wanawake wenye mafanikio, hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi au hajishughulishi.

9: Anayeweza kuwa mlezi wa familia

Ingawa wanawake wengi huwa katika viwango sawa na wanaume wao kwenye elimu na hadhi ya kazi, wanaume huangalia wanawake wanaoweza kugawanya kazi za ofisini na nyumbani pia.

8: Mwonekano Mzuri

Muonekano wa wanawake umezidi kuwa muhimu kwa wanaume kwa muda mrefu. Wengi hupendelea muonekano mzuri na wa kuvutia kutoka kwa wanawake.

7: Afya Bora

Wanaume huangalia pia afya njema kwa mke mtarajiwa, ingawa haipewi msisitizo zaidi kama ilivyokuwa zamani. Afya njema imekuwa moja ya kiashiria cha ndoa ya muda mrefu pamoja na uwezekano wa kuepusha athari za magonjwa ya kurithi kwa watoto.

6: Rafiki

Wanaume na wanawake wanaamini kuoa au kuolewa na mtu ambaye wanapatana vizuri, huchangia kuishi maisha mazuri yenye maelewano ndani ya ndoa.

5: Tabia

Wanaume wameijumuisha tabia njema ya mwanamke katika sifa zao tano bora tangu miaka ya 1930.

4: Elimu na Akili

Elimu na akili ya mwanamke huwavutia wanaume kuliko hapo awali hasa kwa kipindi hiki ambacho wanawake wengi ni wasomi na wafanyakazi. Wanaume wanatafuta wanawake wenye akili na elimu kwaajili ya ustawi mzuri wa familia hapo baadaye.

3: Utulivu wa Kihisia na Ukomavu

Linapokuja suala la mke mtarajiwa, wanaume wanataka mwanamke anayejitambua, aliye na misingi mizuri na mwenye usalama ndani yake.

2: Anayetegemeka

Kama ilivyo kwa wanawake, wanaume pia wanataka mwenzi wa maisha ambaye atakuwa mwaminifu na anayetegemeka. Wanataka mke ambaye atasimama upande wao na katika kila hatua.

1: Upendo

Katika karne ya 20, kutegemewa, kukomaa kihisia na tabia njema vilichukua nafasi za juu kuliko upendo. Sasa, wanaume na wanawake wanaipa nafasi upendo zaidi ya vyote.

Send this to a friend