Vigezo 6 vinavyozingatiwa kwa wagombea uchaguzi Simba SC

0
37

Kamati ya Uchaguzi Simba imesema yeyote ambaye anagombea nafasi ya Uenyekiti wa Klabu ni lazima awe na angalau shahada na lazima awe na uwezo ama haiba ya kuwakilisha klabu ndani na nje ya nchi.

Akitoa taarifa hiyo kwa wapenzi na wanachama wa Simba, Mwenyekiti wa Kamati, Boniface Lyamwike amesema uchaguzi wa Simba utafanyika Januari 29, 2023 na kutaja vigezo mbalimbali vya wagombea wa nafasi zinazowaniwa.

“Anayegombea nafasi ya ujumbe wa bodi ya wakurugenzi lazima awe amefika kidato cha nne na cheti cha kuhitimu, kigezo kingine awe mzoefu wa angalau miaka mitatu ya uongozi wa mpira wa miguu,” amesema Lyamwike.

Ameongeza kuwa kigezo kingine asiwe mmiliki, mwanahisa au kiongozi wa timu nyingine ya mpira wa miguu, pia asiwe amepatikana na hatia ya kosa la jinai, na angalau awe na miaka 25 na si zaidi ya miaka 64.

Send this to a friend