Vigezo vilivyozingatiwa na CAF kuchagua mwenyeji wa AFCON

0
60

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza rasmi kuwa Tanzania, Kenya na Uganda zimepata nafasi ya kuandaa michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027 na kuzishinda Misri, Senegal, Botswana na Algeria huku Morocco ikitangazwa kuwa wenyeji wa michuano hiyo kwa mwaka 2025.

Taarifa hiyo imetolewa leo Jijini Cairo nchini Misri ambapo mkutano wa kamati tendaji ya CAF ulifanyika ili kuamua ni mataifa yapi yatapata uenyeji kwa mwaka 2025 na mwaka 2027.

Kulingana na CAF, viwanja vya mechi vya nchi mwenyeji au nchi wenyeji vinapaswa kuwa karibu na uwanja wa ndege, hospitali ya kiwango chenye hadhi, na hoteli ya nyota tano. Mwenyeji/Wenyeji pia wanapaswa kuwa na viwanja sita vya mpira wa miguu ili kuwahudumia timu 24 zinazoshiriki katika mashindano.

Uwanja wa Benjamin Mkapa National Stadium uliopitishwa na CAF tayari umethibitishwa kwa ajili ya Tanzania huku viwanja vingine vya Azam Complex na CCM Kirumba vikitajwa kuwa sehemu ya mashindano hayo.

Wakati huo huo, Serikali ipo katika mchakato wa kujenga viwanja viwili vyenye uwezo wa kuchukua watu 30,000 kila kimoja, jijini Dodoma na Arusha, ambavyo vinatarajiwa kukamilika kabla ya mashindano hayo.

Skendo 10 za wasanii zilizotikisa dunia

Zaidi ya hayo, kulingana na mahitaji ya CAF, kila nchi mwenyeji zinazojiunga na mashindano inapaswa kuwa na viwanja angalau vitatu vya mazoezi karibu na viwanja vya mechi ambavyo vinakidhi viwango vya CAF. Pamoja na mambo mengine, viwanja vyote vinapaswa kuwa na milango ya kutokea kwenye malango yote pamoja na kamera za za ulinzi (CCTV).

Viti vya VIP na VVIP vilivyofungwa lazima viwe vimepangwa vizuri pamoja na eneo la vyombo vya habari na chumba cha mkutano wa waandishi wa habari kinachoweza kuhudumia waandishi wa habari 50.

Eneo la mchanganyiko, eneo la wapigapicha, eneo la gari la kurushia matangazo (OB van), na chumba cha uendeshaji wa VAR ni mahitaji mengine muhimu.

Kenya ilishinda zabuni za kuandaa mashindano ya AFCON mwaka 1996 pamoja na fainali za Mashindano ya Afrika ya Mataifa ya Mwaka 2018, lakini katika vigezo vya FIFA, viwanja kadhaa vilikuwa havijakamilika na haki za kuwa mwenyeji iliondolewa.

Send this to a friend