
Jeshi la Polisi Mkoa wa Polisi Tarime-Rorya linawashikilia vijana 12 kwa kosa la kufanya fujo na kufunga barabara katika Mji wa Sirari.
Taarifa ya jeshi hilo imeeleza kuwa vijana hao walichukua hatua hiyo baada ya polisi kuwakamata watu wawili.
“Baada ya vijana hao kufikishwa kituoni, vijana wa bodaboda waliopewa taarifa potofu, na ambao walishuhudia watuhumiwa hao kufikishwa kituoni, walirudi eneo la Mji wa Sirari na bila halali yoyote na kwa makusudi, wakajaribu kufanya fujo na kufunga barabara,” imesema.
Aidha, Jeshi la Polisi limetoa onyo kali kwa wote wanaokiuka sheria kuacha mara moja, likisema kuwa halitasita kuchukua hatua kali kwa mujibu wa sheria.







