Vijana milioni 1.7 Tanzania hawana ajira

0
39

Serikali imesema takwimu za utafiti uliofanyika mwaka 2021 unaonesha vijana milioni 1.7 nchini hawana ajira ambao ni sawa na asilimia 12.2 ya nguvu kazi ya vijana milioni 14.2 wenye uwezo wa kufanya kazi.

Ameyasema hayo bungeni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Patrobas Katambi wakati akijibu swali la mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina ambaye aliuliza idadi ya vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 35 ambao hawana ajira, na Serikali imejiandaaje katika ushindani wa soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Naibu Waziri Katambi amesema katika kuhakikisha kuwa vijana wanaandaliwa ipasavyo kushindana katika soko la ajira la ndani na nje, Serikali kupitia wizara yake inatekeleza mkakati wa Taifa wa kukuza ujuzi wa miaka 10 (2016/2017- 2025/2026).

Mwanamke aishi na wembe tumboni kwa miaka 11

Amefafanua kuwa kupitia mkakati huo, Serikali imefanya maboresho ya miundombinu na mitaala katika ngazi za elimu ya juu, elimu ya kati na mafunzo ya ufundi stadi, na kwamba inatoa mafunzo ya kuwawezesha vijana walio nje ya mfumo rasmi wa mafunzo ili kumudu ushindani katika soko la ajira yakiwemo mafunzo ya uanagenzi na mafunzo ya uzoefu wa kazi kwa wahitimu.

Ameongeza kuwa mafunzo mengine ni ya urasimishaji ujuzi uliopatikana nje ya mfumo rasmi wa elimu na mafunzo (RPL) na ya kilimo cha kisasa kwa kutumia teknolojia ya vitalu nyumba.

Send this to a friend