Vijana wanufaika na programu ya Rais Samia katika mifugo

0
40

Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea kuboresha zaidi sekta ya mifugo pamoja na kuwezesha vijana kufikia malengo yao kupitia sekta hiyo.

Akizungumza wilayani Misungwi mkoani Mwanza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi madume ya ng’ombe 36 aina ya boran Heifer kwa halmashauri ya Buchosa, Ulega amesema lengo la serikali ni kuona vijana wanafanya uzalishaji wa mali kwa kuingia katika sekta ya mifugo na kupeleka mifugo hiyo sokoni.

‘’Nchi yetu ina ng’ombe milioni 33 na bado tija ipo chini sana kutokana na viwanda vingi havipati malighafi ya kutosha. Mifugo inatakiwa kuongeza tija na pato la taifa na kwa mtu mmoja mmoja’’ amesema.

Ameongeza kuwa kupitia programu maalum ya Samia Ufugaji kwa Tija (SAUTI), serikali imefanikisha kuanzisha mafunzo ya unenepeshaji mifugo ambapo takribani vijana 70 wanapatiwa mafunzo hayo kwa vitendo katika Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) wilayani Misungwi.

Send this to a friend