Vijana wapewa mikopo takribani bilioni 2

0
22

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana imetoa mikopo yenye thamani ya TZS bilioni 1.88 kwa ajili ya kuwezesha miradi 85 ya vijana katika sekta za kilimo, viwanda na biashara kwenye halmashauri 28.

“Ni ukweli usiopingika kuwa suala la uwezeshaji wa vijana ni muhimu katika kukuza uchumi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba vijana ni nguvu kazi inayotegemewa na ni kundi kubwa katika nchi yetu. Kwa msingi huo maendeleo yetu yanategemea sana vijana kwani hili ni kundi kubwa na muhimu lenye umri wa kufanya kazi. Wingi wa vijana wenye ujuzi, ni chachu ya kuharakisha maendeleo endelevu,” amesema.

Waziri Mkuu: Tumeanza kuifanyia kazi ripoti ya CAG

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wote zikiwemo taasisi za kifedha, mashirika ya kimataifa na sekta binafsi katika kujenga nguvu kazi yenye ujuzi itakayoshiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya taifa.

Aidha, amebainisha kuwa, tangu Serikali ianze kutekeleza programu ya taifa ya Kukuza Ujuzi, imetoa fursa za mafunzo ya ujuzi wa kujiajiri au kuajiriwa kwa vijana 118,415 katika fani za uanagenzi, uzoefu wa kazi, ufugaji wa samaki na viumbe maji na kilimo cha kisasa kwa njia ya vizimba.

Waziri Mkuu amewataka vijana waendelee kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa za uwepo wa mradi mbalimbali ya kuinua vijana kiujuzi na kiuchumi.

Send this to a friend