Vikosi 10 vyenye wachezaji ghali zaidi AFCON 2023

0
62

Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), ambalo ni mashindano makubwa ya soka barani Afrika, limeanza nchini Ivory Coast. Mashindano haya ya heshima, yanayoidhinishwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), yamekuwa burudani ya soka tangu kuanzishwa kwake mwaka 1957.

Toleo la kwanza la AFCON lilishirikisha nchi tatu, lakini miaka 67 baadaye, idadi ya washiriki imeongezeka zaidi, na sasa timu 24 zinapambania ubingwa huku mshindi kujinyakulia Dola milioni 7 [TZS bilioni 17.6], na mshindi wa pili akichukua Dola milioni 4 [TZS bilioni 10], mshindi wa tatu kupata Dola milioni 2.5 [TZS bilioni 6.5], na timu itakayoshika nafasi ya nne itapata Dola milioni 1.3 [TZS bilioni 3.3].

Orodha ya wachezaji bora wa ligi kuu Tanzania mwaka 2013-2023

Kulingana na ripoti ya Bettingsites.co.uk, Super Eagles ya Nigeria ndiyo timu yenye thamani kubwa zaidi katika mashindano haya. Wana wachezaji wengi wanaocheza katika ligi kuu za Ulaya, na mshambuliaji wao wa Napoli, Victor Osimhen akiwa ndiye mchezaji ghali zaidi katika kikosi hicho.

Vifuatavyo ni vikosi 10 vyenye wachezaji ghali zaidi kwenye mashindano ya AFCON 2023;

  1. Nigeria: TZS bilioni 960
  2. Morocco: TZS bilioni 952.4
  3. Ivory Coast: TZS bilioni 916.7
  4. Senegal: TZS bilioni 752.1
  5. Ghana: TZS bilioni 538
  6. Algeria: TZS bilioni 516
  7. Mali: TZS bilioni 384.3
  8. Cameroon: TZS bilioni 376
  9. Misri: TZS bilioni 370.5
  10. DR Congo: TZS bilioni 301.9

Chanzo: Business Insider

Send this to a friend