Vioja: Wavunja duka na kuiba viatu 200 vyote vya mguu wa kulia

0
77

Polisi nchini Peru wanawasaka watu watatu wanaodaiwa kuvamia duka moja katikati mwa jiji la Huancayo na kuondoka na viatu zaidi ya 200 vyenye thamani ya TZS milioni 30, lakini vyote vya mguu wa kulia.

Kwa mujibu wa ripoti ya BBC, kamera za CCTV kutoka dukani humo zimewanasa wahalifu hao wakivunja kufuli usiku wa manane, siku ya Jumapili Mei 02, mwaka huu na kuondoka na masanduku ya viatu vya chapa tofauti za kimataifa.

Mwanasiasa afungwa kwa njama za kuiba figo

Akizungumza Mkuu wa Polisi wa eneo hilo, Eduan Diaz ameviambia vyombo vya habari vya Peru kuwa tayari wamekusanya ushahidi kutoka katika eneo hilo ikiwemo picha na alama za vidole zinazodhaniwa kuwa ni za watuhumiwa hao.

“Tumekusanya ushahidi katika eneo la tukio, kwa picha na alama za vidole, tutaweza kuwapata watu hao,” amesema.

Send this to a friend