Viongozi wa CHADEMA wakamatwa kwa mkusanyiko usio halali

0
37

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya, Masaga Pius Kaloli mkazi wa Wilaya ya Chunya na Mwenyekiti wa BAVICHA mkoani humo, Elisha Chonya mkazi wa Makunguru kwa tuhuma za kuhamasisha watu kufanya mikusanyiko isiyo halali.

Taarifa ya Polisi imesema watuhumiwa walikamatwa Januari 21, 2026 katika Kijiji na Kata ya Inyala, mkoani humo baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za uwepo wa viongozi hao waliokuwa wakifanya maandalizi na kuhamasisha watu kukusanyika kwa ajili ya mkutano.

“Ikumbukwe kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimezuiliwa na Mahakama kufanya shughuli zozote za kisiasa,” imeeleza taarifa ya Jeshi la Polisi.

Aidha, polisi wamesema upelelezi unakamilishwa ili hatua zaidi za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao.

Send this to a friend