Viongozi wa dini waliombea taifa amani

0
40

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla amekutana na viongozi wa dini na wa kimila kutoka Mkoa wa Arusha na kushiriki sala na dua maalum ya kuliombea taifa pamoja na viongozi wakuu wa nchi.

Makalla amesisitiza umuhimu wa viongozi hao kuendelea kuhubiri amani na kushirikiana na waumini wao kuliombea taifa.

“Muhimu kuhubiri kuwa hakuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania na ili tusonge mbele katika maendeleo ni muhimu kuendelea kuwa na amani na utulivu kwahiyo kila mmoja wetu arejeshe matumaini na maombi hayo kwamba Watanzania tunahitaji amani hivyo sala na maombi yetu kwa Mwenyenzi Mungu ni amani na sisi serikali tutaendelea kupokea ushauri wenu na kuufanyia kazi,” amesema.

Makalla kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ameahidi kuendelea kutekeleza wajibu wake wa msingi wa kuhakikisha wanalinda raia na mali zao pamoja na kuendelea kupokea maoni na ushauri kutoka kwa viongozi wa dini na jamii ili kuhakikisha utulivu na usalama unabakia kuwa msingi wa maendeleo ya Tanzania.

Send this to a friend