Viongozi wa dini waungana kumuombea Rais Samia kwa kudumisha amani

0
85

Viongozi wa dini wa Mkoa wa Kagera wameungana kwa pamoja kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine wa kitaifa kwa kuendelea kudumisha amani, utulivu, upendano na maelewano.

Ibada hiyo iliyowakutanisha viongozi wa Dini ya Kikristo na Kiislamu imefanyika leo katika Kanisa Anglikana Mt. Yohana Kimbugu, Muleba mkoani Kagera iliyoambatana na Harambee ya Ujenzi wa Kanisa.

Akiongoza ibada hiyo, Askofu wa Dayosisi ya Lweru Kanisa la Anglikana Tanzania, Godfrey Mbelwa amesema viongozi wa dini na waumini wana wajibu wa kuwaombea viongozi wa Kitaifa kwakuwa wanafanya kazi kubwa ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Aidha, katika Harambee ya Ujenzi wa Kanisa, Waziri Bashungwa amewasilisha mchango wa viongozi wa Serikali Shilingi milioni 30 na kuahidi kuendelea kushirikiana na viongozi wa Kanisa hilo ili ujenzi ukamilike kwa wakati.

Send this to a friend