Viongozi wa makanisa wasema anayejiita ‘Yesu wa Tongaren’ ni tapeli

0
50

Waumini wa makasisi kutoka kaunti ya Bungoma nchini Kenya wamekemea na kulaani kitendo cha mtu anayejiita ‘Yesu wa Tongaren’ wakimtaja kuwa mtu huyo ni mwongo na tapeli.

Waumini hao wakiwa pamoja na viongozi wa dini wamedai mtu huyo amekwenda kinyume na maandiko matakatifu na wanataka kukomesha kile wanachokiona kwa kuwa ni chukizo katika dini ya Kikristo.

“Sisi ni wafuasi wa Yesu na hakuna mwanadamu anayeweza kuwa Yesu, tunaomba ulimwengu wote kwa ujumla uliosikia upotofu huu, ijiepushe na kusikia upotovu huu, hawa ni watu ambao hawaelewi biblia kabisa,” amesema Askofu Calistus Barasa.

Askofu Barasa amebainisha kuwa watu hao wanaopotosha ulimwengu wakijiita majina ya manabii hawajulikani hata katika makanisa na viongozi wa dini hivyo husumbuliwa na njaa tu kwa kujificha katika kivuli hicho.

Mume ajinyonga ukweni baada ya mkewe kugoma kurudi nyumbani

“Tunasikia watu wanaojilinganisha na Yesu, sisi kama kanisa hatuwatambui hata kidogo” ameongeza Mchungaji Fredrick Ogara.

Hivi karibuni mwanaume aitwaye Eliud Wekesa kutoka kijiji cha Lukhokwe, eneo la bunge la Tongaren huko Bungoma aligonga vichwa vya habari akijiita ‘Yesu wa Bungoma’ (Yesu wa Tongaren) na kujaribu kuiga mambo aliyoyafanya Yesu kama ilivyoandikwa kwenye biblia.

Send this to a friend