Ethiopia yaweka zuio utoaji wa shahada za udaktari wa heshima, na matumizi ya cheo cha ‘Daktari’

0
115

Wizara ya Elimu nchini Ethiopia imepiga marufuku wapokeaji wa shahada za udaktari wa kutumia cheo cha “Daktari” au “Dr” nje ya taasisi walizopewa heshima hiyo.

Aidha, agizo hilo limeweka wazi kuwa viongozi wa serikali waliopo madarakani pamoja na wagombea wa kisiasa hawataruhusiwa kupokea shahada hizo.

Kwa mujibu wa mwongozo huo, vyuo vikuu vipya havitaruhusiwa kutoa shahada za udaktari wa heshima hadi pale vitakapohitimu angalau makundi nane ya wanafunzi na kuanza kutoa shahada za ngazi ya juu zaidi, ikiwemo PhD.

Sharti hilo limekusudiwa kuhakikisha kuwa ni taasisi zilizokomaa na zinazokidhi viwango vya kitaaluma pekee ndizo zitakazoruhusiwa kutoa heshima hizo.

Hata hivyo, Shahada za heshima za udaktari zitaruhusiwa kutolewa kwa raia wa Ethiopia au wageni waliotoa mchango mkubwa katika taaluma zao. Zinaweza pia kutolewa kwa mtu mmoja au kikundi, hai au kilichokwisha kufariki, iwapo kimekidhi vigezo vilivyowekwa.

Send this to a friend