Viongozi wa zamani wa Sekretarieti ya CHADEMA watangaza kujiondoa CHADEMA

0
4

Baadhi ya viongozi wa zamani wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa wakiongozwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Benson Kigaila wametangaza kuachana na chama hicho, wakieleza kutoridhishwa na mwenendo wa mambo ndani ya chama.

Miongoni mwa viongozi hao ni wale wanaohusishwa na kundi la CHADEMA G-55, linalojulikana kwa msimamo wake na ukosoaji ndani ya chama hicho.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, viongozi hao wamesisitiza kuwa bado wana nia ya kuwatumikia Watanzania, japokuwa hawajafafanua rasmi kwa njia ipi.

Wanachama hao akiwemo, Catherine Ruge na John Mrema wamesema maamuzi yao yamesababishwa na kile walichokiita ukiukwaji wa haki na mwelekeo usioimarisha chama.