Mratibu wa kukinga na kudhibiti maambukizi Wizara ya Afya, Dkt. Joseph Hokororo amesema mgonjwa wa Ebola anapopona, bado anaweza kuambukiza mtu mwingine kupitia mbegu za kiume na mwanamke anaweza kumwambukiza mtu mwingine kupitia matiti kwa kipindi cha miezi sita.
Ameyasema hayo leo Desemba 10, 2022 wakati akizungunza na waandishi wa habari na kutoa elimu kuhusu ugonjwa wa Ebola.
Dkt. Hokororo ameeleza kuwa ingawa ugonjwa huo haujachukuliwa kama maradhi yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana (ngono), katika baadhi ya tafiti wataalamu wamebaini kuwa virusi vyake vinaweza kusambazwa kwa njia hiyo hata baada ya wagonjwa kupona.
Watafiti wabaini kupungua kwa manii kwa wanaume
“Virusi vya Ebola husalia ndani ya mbegu za uzazi za kiume hata baada ya mgonjwa kupona kwa kuwa licha ya matibabu virusi hivyo haviwezi kuondoka kwa haraka katika manii na hivyo mgonjwa anaweza kusambaza virusi kwa mtu mwingine kwa njia hiyo.
“Kwa mwanamke anaweza kumwambukiza mtoto anayemnyonyesha kupitia matiti yake au iwapo mwanaume atanyonya matiti yake,” amesema.
Aidha, mefafanua kuwa maumbile ya virusi vya Ebola yanaipa uwezo wa kuishi kwa muda mrefu kwenye ubongo, uti wa mgongo, mbegu za kiume, nyumba ya uzazi na kwenye macho, hata baada ya mgonjwa kuthibitishwa amepona, na virusi hivyo vinaweza kuishi katika mbegu za kiume kwa muda mrefu kuliko majimaji ya mwili.