Visababishi 6 vya kichomi  kifuani

0
123

Kichomi ni maumivu makali ya ghafla yanayotokea na kupotea ndani ya muda mfupi sana. Kwa kawaida vichomi vinaweza kutokea sehemu yoyote ya mwili, pia maumivu yanaweza kusafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa haraka mithili ya kupigwa shoti ya umeme.

Haya ni mambo ambayo yanaweza kusababisha kupata kichomi kifuani;

•Matatizo ya moyo
•Wasiwasi uliopitiliza na mshiko wa hofu
•Matatizo ya kifua na upumuaji
•Magandamizo, kuteguka kwa misuli au maumivu ya mifupa ya kifua
•Kucheua tindikali (udhaifu unaotokana na kushindwa kufanya kazi kama inavyotakiwa kwa koki inayoruhusu chakula kuingia tumboni).
•Magonjwa mengine (magonjwa haya yanaweza kuwa mkanda wa jeshi, degedege, michomo kwenye kongosho, madhaifu ya umezaji chakula n.k)

Namna 5 ya kuepuka kupwa na kiharusi

Kama unapata maumivu yanayoambatana na dalili zifuatazo ni vyema kufika kituo cha afya kwa ajili ya uchunguzi;

•Kutokwa jasho sana
•Kichefuchefu
•Maumivu yanayosambaa shingoni au kwenye taya
•Maumivu yanayosambaa kwenye mabega, mikono au mgongoni
•Kizunguzungu au kuhisi kichwa chepesi
•Kuishiwa pumzi
•Kuzimia au mapigo ya moyo kupiga kwa nguvu

Unashauriwa kuonana na mtaalamu wa afya endapo dalili unayoipitia inatia hofu ili kufanya uchunguzi zaidi.

Chanzo: ULY Clinic

Send this to a friend