Vita ya Ronaldo na Messi yahamishiwa Klabu Bingwa Ulaya

0
54

Christiano Ronaldo na Lionel Messi watakutana tena katika mzunguko wa 16 bora wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) baada ya vilabu vya  PSG na Manchester United kupangwa pamoja.

Miamba hiyo miwili ya soka itakutana tena dimbani kutunishiana misuli wakikumbushiana zama za Hispania kabla ya Ronaldo kutimkia Juventus.

Timu hizo mbili zilikutana pia msimu uliopita ambapo baada ya michezo yote miwili PSG iliibuka na ushindi wa magoli 4-3.

Mchezo mwingine unaosubiriwa kwa hamu kwenye mzunguko huo ni Atletico Madrid dhidi ya Bayern Munich.

Image

Send this to a friend