Vitabu 5 vinavyosomwa zaidi Afrika

0
35

Usomaji wa vitabu ni njia nzuri ya kujifunza na hata kubadili maisha yako kwa ujumla, ambapo husaidia kukupa ujasiri wa kujenga hoja na kukupa mawazo mapya.

Business Insider Afrika imetoa orodha ya vitabu vitano vilivyoandikwa na waandishi mahiri kutoka barani Afrika ambavyo vinatoa mitazamo ya kipekee na masimulizi yenye nguvu.

Fuatilia vitabu hivi vitano vinavyokubalika zaidi Afrika;

1. Dear Ijeawele, or a Feminist Manifesto in Fifteen Suggestions: Mwandishi Chimamanda Ngozi Adichie (Nigeria)

Mwandishi mashuhuri wa Nigeria anawasilisha mawazo yenye nguvu kwa njia ya barua. Kitabu cha Adichie ambacho kinaelezea utamaduni wa kiigbo wa nchini Nigeria kinahamasisha na kukuza usawa wa kijinsia.

2. The African Origin of Civilization: Myth or Reality: Mwandishi Cheikh Anta Diop (Senegal)

Cheikh Anta Diop, mwanahistoria anayeheshimika nchini Senegal, anafanya vizuri katika kitabu cha Diop ambacho kinaendelea kuwavutia wasomaji juu ya urithi wa Kiafrika na athari zake za kudumu kwa binadamu na jamii.

3. Palace Walk / Palace of Desire / Sugar Street: Mwandishi Naguib Mahfouz

Mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Misri, Naguib Mahfouz anatupeleka katika safari ya vizazi vitatu vya familia ya Cairo. Akikabiliana na hali ya mabadiliko ya kisiasa na kijamii nchini Misri mwanzoni mwa karne ya 20, Mahfouz anatunga kwa ustadi hadithi ya upendo, usaliti na uthabiti, akiwapa wasomaji maarifa ya kina kuhusu jamii ya Misri.

4. Homegoing: Mwandishi Yaa Gyasi (Ghana)

Kitabu cha Homegoing cha Yaa Gyasi kinaeleza maisha ya dada wawili wa kambo na vizazi vyao, kuanzia Ghana ya karne ya 18 hadi Amerika ya kisasa. Gyasi anaonesha urithi wa utumwa na matokeo yake kupitia simulizi zilizounganishwa ambazo zinachunguza utambulisho, familia na athari za kudumu.

5. Wizard of the Crow: Mwandishi Ngũgĩ wa Thiong’o (Kenya)
Ngũgĩ wa Thiong’o, mwandishi mashuhuri wa Kenya, anawasilisha hadithi ya kejeli ya kuvutia ambayo inachanganya uhalisia wa kichawi na ufafanuzi wa kisiasa ikieleza ufisadi na changamoto zinazowakabili watu wa kawaida.