Vitambulisho milioni 10 kuanza kutolewa Januari 2023

0
60

Serikali kupitia Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini imesema vitambulisho vya taifa milioni 10 vitaanza kutolewa kuanzia Januari mwakani.

Ameyasema hayo kwenye mkutano wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kigoma Vijijini katika mazungumzo ya njia ya simu na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Christina Mdeme.

Sagini amesema Serikali imetenga shilingi bilioni 42 kwaajili ya kushughulikia uchapaji na upelekaji wa vitambulisho hivyo kwa wananchi, na kwamba changamoto ya UVIKO-19 ilikuwa moja ya sababu iliyokwamisha uchapishaji, kwakuwa viwanda vya malighafi za kutengenezea vitambulisho vilifungwa.

“Pia tulikuwa na changamoto ya mkataba na mkandarasi aliyepewa kazi ya kutengeneza vitambulisho, lakini tumeshafikia suluhisho na kazi itaanza mara moja,” amesema Sagini.

Send this to a friend