Vitendo vya wizi Dar vyamshitua Rais Samia, atoa agizo

0
56

Rais Samia Suluhu Hassan ameonya dhidi ya vitendo vya ujambazi na wizi vilivyoanza kujitokeza katika Mkoa wa Dar es Salaam na amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kudhibiti vitendo hivyo mara moja.

Ametoa agizo hilo leo Mei 7, 2021 wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam kwa niaba ya wazee wote wa Tanzania.

Amesema kuwa kwa siku za hivi karibuni vitendo hivyo vimeanza kushamiri huku akiwataka watu wanaotekeleza vitendo hivyo vya kihalifu kuacha mara moja kujaribu kina cha maji.

Aidha, ametoa wito kwa wazee hao na wazazi wote nchini kuwalea vijana wao katika maadili mema ili watambue wajibu wao kwa wazee, nidhamu na heshima kwa jamii na kuwajali Wazee na kuacha tabia zisizokubalika kwenye jamii.

Send this to a friend