Vitu 9 zaidi ya uzuri wa mwanamke ambavyo wanaume hupendelea

0
76

Vitu ambavyo wanaume hupenda mara nyingi havina uhusiano wowote na jinsi mwanamke anavyoonekana au vitu vyovyote ambavyo tunadhani wanaume hupenda kwa mwanamke. Japokuwa ni kweli muonekano wa mwili ndio cha kwanza wanachokiona, ila ikifikia katika kutaka kuishi na mwanamke, muonekano na maumbile ya mwanamke huwa ni kitu cha mwisho kabisa kufikiriwa na mwanaume.

Vifuatavyo ni vitu 9 ambavyo mwanaume huviangalia sana atakapofikia hatua ya kutaka kuishi na mwanamke.

Msikivu / anayesikiliza. Wanaume wengi hupenda sana kusikilizwa. Sauti yake iwe ndo yenye amri yamwisho. Hivyo mwanamke msikivu huwa na nafasi zaidi.

Aliyeridhika au kujitosheleza. Wanawake wanaofurahia wanachokifanya ni wazuri zaidi. Ina maana kwamba wanawake inawabidi waache kulalamika kuhusu vitu wasivyonavyo na waanze kufurahia vile walivyonavyo. Haijalishi una uzuri kiasi gani, una kazi nzuri kiasi gani, au una CV yenye ukubwa upi, bali hili linagusia wewe kuwa na furaha na jinsi ulivyo kama mwanadamu. Na vile vile ni jinsi ulivyo na mtazamo chanya kwamba wewe ni mwanamke mahiri na unayestahili vitu vizuri.

Mpishi mzuri. Mabibi zetu walikuwa wakisema njia ya pekee kuukonga moyo wa mwanaume ni kwa kupitia tumbo lake, kila mtu anakumbuka hili. Siku hizi Wanawake kila kitu anaachiwa dada wa kazi. Unamfanyia hivyo mchumba sasa hivi, anakuchora tu….

Kuwa wa kweli. Japokuwa wasichana ambao wamejitengeneza wanageuza sana shingo za watu, na kupata vinywaji vya bure. Wanaume wengi wanakubaliana kwamba hawawezi kamwe kumchagua mwanamke kama huyo kwa ajili kitu zaidi mapenzi ya kawaida. Kucha bandia, nywele za bandia, kope za bandia, kila kukicha amejipodoa, hiyo ni gharama ambayo hamna mwanaume anataka kuibeba maishani mwake.

Utayari wa kufikia muafaka: Kila mwanaume anajisikia vizuri akiwa anajua kwamba mwanamke wake yuko tayari kufanya makubaliano na vile vile anajitihada za kutafuta suluhu ambazo zitakubalika pande zote mbili.

Mcheshi: Kama ana mpango wa kuishi na wewe basi angalau atahakikisha umcheshi kidogo, maana kununiana ndani ya nyumba sio vizuri. Na vile vile watu wengi huhusisha ucheshi na uwezo wa mkubwa wa akili.

Ujasiri: Ni mojawapo ya vitu ambavyo wanaume wengi hupenda kwa mwanamke, hii humpa moyo kwamba hata katika hali ambayo yeye hatakuwepo, mwanamke wake atamsaidia katika maamuzi.

Kutokua feki kila wakati: Make up sawa inapendwa, lakini sasa isiwe maisha yako mpaka unasahaulika unakuaga vipi ukiwa Natural.

Mchakarikaji ikifikia katika ule muda muafaka: Mwanamke asie muoga na mwenye kujiweza na kujituma ikifikia wakati wa kuridhishana ni nyoongeza ya kutosha kwa mwanaume endapo wewe ndiyo amekuchagua kuishi naye.

Send this to a friend