VODACHAT: Zijue Fursa za Uwekezaji Kidjitali

0
3

Vodacom Tanzania PLC kupitia jukwaa lake la VODACHAT imeendesha mjadala wa moja kwa moja kuhusu Fursa za Uwekezaji Katika Dunia ya Kidijitali, ukihusisha wataalam wa sekta ya uwekezaji na teknolojia. Zaidi ya watu 5,200 walijiunga kupitia X Space (zamani Twitter) na Facebook, wakishiriki mijadala yenye tija kuhusu namna na njia bora za kuwekeza kidijitali.

Mtaalam wa uwekezaji, Edmund Munyagi ameeleza kuwa uwekezaji wa kidijitali unatoa fursa kama kununua hisa mtandaoni, biashara ya fedha za mtandaoni, uwekezaji katika mtindo wa faida kuzaa faida (compound interest) na crowdfunding. Hata hivyo, ameonya kuwa fursa hizo pia zinakuja na changamoto kama ukosefu wa elimu ya fedha, ambapo Watanzania asilimia 1.4 tu wamewekeza katika fursa hizo.

Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), CPA Alfred Mkombo, amebainisha kuwa, kwa sasa Tanzania ina mazingira mazuri ya uwekezaji, akiongeza kuwa pamoja na idadi ndogo ya wawekezaji, asilimia 98 ya wawekezaji ni Watanzania huku asilimia 64 wakiwa ni wawekezaji wa mtu mmoja mmoja.

Amesisitiza umuhimu wa suluhisho bunifu kama M-Wekeza, ambalo linatoa fursa rahisi za uwekezaji kwa kila Mtanzania.

Epimack Mbeteni, Mkurugenzi wa M-Pesa – Vodacom Tanzania, alieleza jinsi M-Wekeza inavyorahisisha uwekezaji kwa njia salama na ya kidijitali. “Kwa kuanza na TZS 1,000 tu, kila Mtanzania anaweza kuanza safari ya uwekezaji na kufaidika na riba ya 13% kwa uwekezaji wake.”

Kupitia M-Pesa, Vodacom Tanzania inaendelea kuongeza ujumuishwaji wa kifedha kwa kutoa huduma kama mikopo ya simu, bima mbalimbali na mikopo ya pesa taslimu kwa wateja wake.

Je, umeanza safari yako ya uwekezaji wa kidijitali?

Send this to a friend