Vodacom Tanzania yafungua duka jipya Dodoma

0
43

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Philip Besiimire amezindua duka kubwa jipya la mfano la kampuni hiyo mkoani Dodoma ambalo litasaidia kutoa huduma kwa wateja wa mkoa huo pamoja na mikoa mingine ya kanda ya Kati.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC Philip Besiimire ( wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa duka jipya la Vodacom jijini Dodoma, ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kampuni hiyo karibu na wateja wa jiji hilo. Tukio hilo lilishuhudiwa na Mkuu wa kanda ya kati, Chiha Nchimbi (wa pili kulia) pamoja na Mdau wa Vodacom Emmanuel Makaki ( Kushoto) jana jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa uzinduai wa duka hilo, Besiimire amesema duka hilo ni mkombozi kwa wakazi wa Mkoa wa Dodoma na mikoa jirani iliyo katika Kanda ya Kati kutokana na kuboreshwa kwa huduma zake ikiwemo huduma ya wateja wenye mahitaji maalumu wakiwemo viziwi, walemavu wa miguu, macho na wengineo huduma ambayo hapo awali haikuwepo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire (wa pili kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa watoa huduma wa duka jipya kubwa la Vodacom mkoani Dodoma baada ya kulizindua jana. Kulia ni Mdau wa Vodacom, Emmanuel Makaki, Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kati, Chia Nchimbi (kulia kwake) na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire (wa pili kushoto) akitazama bidhaa zilizopo ndani ya duka jipya kubwa la Vodacom mkoani Dodoma jana baada ya kulizindua. Kushoto ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kati, Chia Nchimbi.

Kwa upande wa wateja wa Vodacom wameishukuru Vodacom kwa uzinduzi wa duka hilo na kusema kuwa kwa sasa watanufaika na huduma zake kutoka na kuboreshwa kwa huduma zake ikiwemo ukubwa wake ukilinganisha na duka la awali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire (kushoto) akitazama moja ya simu zinazouzwa ndani ya duka jipya kubwa la Vodacom mkoani Dodoma baada ya kulizindua jana. Wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa duka hilo.

Send this to a friend