Vodacom waiomba Serikali iangalie suala la tozo bajeti ijayo

0
14

Kampuni ya Vodacom imeiomba Serikali kuangalia upya suala la tozo katika bajeti inayokuja ili kuwasogeza zaidi watumiaji katika mfumo wa kidijitali utakaosaidia kupata mapato mengi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Vodacom, Philip Besiimire wakati akishiriki katika Kongamano la Kodi lililoandaliwa na Wizara ya Fedha Januari 11, 2023 jijini Dar es Salaam.

“Ukifuatilia kodi kwa sasa kulikuwa na matokeo ambayo hayakukusudiwa, kwa mfano nilivyokuwa naangalia kwa uzoefu wa Vodacom kwa mwaka jana au mwaka juzi tulipoleta tozo, tulipoteza watumiaji milioni moja wa M-Pesa, kwa maneno mengine waliondoka katika mfumo wa kidigitali walichukua pesa zao na wakaacha kutumia M-Pesa,” amesema.

Aidha, Besiimire ameishauri Wizara ya Fedha na Mipango kuangalia kiwango sahihi cha kodi kiweje ili  kusaidia kuongeza watumiaji zaidi wa mtandao huo.