Vodacom yazindua “Amsha Ndoto, Amsha Shangwe” promosheni

0
46

·        Mamilioni kushindaniwa hapo kwa hapo, zawadi kila siku na kila wiki 

·        TZ 10ml/ kushindaniwa kila wiki, TZ 5ml/ kila siku

Vodacom Tanzania plc imezindua promosheni ya wiki nane ya msimu wa siku kuu iitwayo “Amsha Ndoto, Amsha Shangwe” itakayowawapa wateja wa Vodacom fursa ya kujishindia zawadi mbali mbali ikiwemo, mshindi mmoja wa Tsh10, 000,000 kila wiki na Tsh1,000,000 kila siku kwa washindi watano. Vile vile wateja watakuwa na nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo simu janja, TV janja, mifumo ya 5G, bima ya VODA BIMA na usafiri wa bure kupitia Paisha.

Masta Shangwe

Wateja wa Vodacom wanaweza kushiriki kwenye promosheni hii na kupata nafasi ya kujjishindia zawadi mbalimbali kwa kufanya manunuzi na miamala kupita M-Pesa kwa kipindi hichi cha promosheni, pamoja na kutumia huduma za usafiri wa Paisha. Miamala yote itakayofanyika kupitia M-Pesa kwa kipindi hichi cha promosheni itaingia kwenye droo na kumpa mteja nafasi ya kushinda.

Mkurugenzi wa biashara Vodacom, Linda Riwa

Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni

Akizunguma kwenye uzinduzi, Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania plc, Philip Besiimire alisema Vodacom imekuwa na utamaduni wa kuwatunuku wateja msimu wa siku kuu kuainisha jinsi Vodacom inathamini mchango wao

Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania plc, Philip Besiimire

“Msimu wa siku kuu ni muhimu na unahamasa kwetu sote. Tunapata fursa ya kupumzika na kuwa na wapendwa wetu vile vile kutafakari mafanikio yetu ya mwaka wakati tunaweka malengo yam waka ujao. Kipindi hiki kawaida tuna utaratibu wa kutembelea familia zetu na kuwanunulia zawadi, na sisi kama Vodacom familia yetu ni wateja wetu na ndio sababu ndani ya miaka michache iliyopita tulianzisha utaratibu wa kuwapa zawadi wateja wetu ili kufanya msimu huu wa siku kuu uwe wa furaha zaidi kwao, alisema Bisiimire.

Alisema Vodacom inamatumaini ya kusaidia kufanikisha ndoto za wateja wake hasa kipindi hichi cha msimu wa siku kuu, ametoa wito kwa wateja wa Vodacom kutumia M-Pesa kufanya miamala na kujiongeea nafasi za kushinda zawadi kubwa.

“Inawezekana ulitaka kumiliki gari, kuanzisha biashara, kulipa ada ya shule, kumalizia ujenzi wa nyumba au kwenda kupumzika, sisi Vodacom tungependa kukusaidia kufanikisha ndoto yako . Tunaamini zawadi tutayokupa utasambaa furaha kwa wateja wetu. Masta Shangwe  wetu atatembelea nnchi nzima kusambaa upendo na furaha, hivyo tunatoa wito kwa wateja wetu kufikiria mbele zaidi na kuamini kuwa wakiwa na Vodacom” alisema Bisiimire.

Send this to a friend