Vunjabei: Jokate ni dada yangu

0
92

Mfanyabiashara maarufu, Fred Vunjabei amefafanua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo ni dada yake tu na si vinginevyo kama ambavyo watu wanasema.

Vunja bei ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa duka lake jipya mkoani Kigoma ambapo kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Jokate.

“Nilishasema na niseme tena, Jokate ni dada yangu, ni kiongozi ambaye ameaminiwa na Rais, anasapoti vijana kama ambavyo na mimi nimekuwa nikifanya. Mwacheni dada wa watu yuko kazini huko atapaliwa bure,” amesema Vunjabei.

Send this to a friend