Vyakula vinavyofaa na visivyofaa kula wakati wa hedhi

0
112

Mei 28 ya kila mwaka ni siku ya kimataifa ya hedhi salama. Jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika duniani kote wakati huu ambapo suala la hedhi linachukuliwa na jamii kuwa ni ugonjwa au mkosi na hivyo kuwakosesha watoto wa kike haki ya kupata huduma ya kujisafi wakati wa mzunguko wa hedhi kila mwezi.

Baadhi ya wasichana na wanawake hupitia changamoto za maumivu makali wakiwa hedhi. Kiuhalisia ni ngumu kuielezea hali wanayopitia wanawake na wasichana katika vipindi vyao vya hedhi, ambapo wakati mwingine hali hiyo hutokana na ulaji usio sahihi.

FLO Heath wanaeleza vyakula vinavyofaa na visivyofaa kuliwa hakati wa hedhi.

Tikitimaji
Sukari asilia inayopatikana katika tunda hili inaweza kutosheleza kuzuia kula vyakula vyenye sukari. Zaidi ya hayo, matunda haya yana vitamini nyingi na maji mengi yatakayosaidia mwili wako kuwa na unyevu ambao utapunguza hali ya uvimbe.

Mayai
Madini ya chuma, mafuta, vitamini B, asidi muhimu ya mafuta, na protini katika viini vya mayai husaidia. Lakini ikiwa una tumbo nyeti, epuka mayai ya kuchemsha, ambayo yanaweza kusababisha gesi, hali ya uvimbe, na kiungulia.

Chokoleti nyeusi
Bila shaka ni moja ya vyakula maarufu zaidi vya kula wakati wa kipindi chako kwa kuwa aina hii ya chokoleti ina magnesiamu nyingi na chuma. Kwa mujibu wa Flo health, chokoleti nyeusi ni chakula kizuri cha faraja. Hata hivyo unashauriwa kula kwa kiasi kwa kuwa ina sukari na kafeini.

Karanga
Karanga nyingi zina asidi nyingi ya mafuta ya omega, pia ni chanzo kikubwa cha protini hivyo hakikisha unakula karanga kila siku unapokuwa kwenye kipindi chako.

Vyakula vya kuepuka

Wakati wa hedhi wanawake na wasichana hupoteza damu na kunakabiliwa na mabadiliko ya haraka ya homoni. Chagua vyakula vyenye virutubishi vya kutosha kama vile vitamini, madini, maji, protini, chuma, na nyuzinyuzi.

Wakati huo huo jaribu uwezavyo kuzuia yafuatayo:

Vyakula vilivyosindikwa
Vyakula vya makopo kama vile nyama iliyochakatwa kwa wingi na vitu vingine vilivyotengenezwa kwa kemikali vinaweza kufanya uvimbe na uhifadhi wa maji kuwa mbaya zaidi. Viwango vya juu vya sodiamu sio vizuri wakati wowote wa mwezi, pia husababisha uharibifu zaidi wakati wa kipindi chako.

Epuka viwango vya juu ya sukari
Kwa mujibu wa Dkt. McClure anasema vyakula vilivyo na sukari na vitamu vitaongeza viwango vyako vya insulini, viwango vyako vya sukari katika damu vinapopanda na kushuka unaweza kuhisi uchovu au kuumwa na kichwa mara kwa mara.

Pombe
Unapokuwa kwenye hedhi, punguza au uondoe matumizi ya vileo. Kwa nini hili ni muhimu? Kupoteza damu hupunguza shinikizo la damu, hivyo matumizi ya pombe yatazidisha uchovu na kuongeza mtiririko wa hedhi.

Vyakula vyenye viungo vingi
Je! Tayari unapambana na uchovu, kutokwa na damu nyingi na tumbo? Kula vyakula vya viungo kunaweza kuongeza gesi na kujihisi vibaya. Ikiwa huwezi kuacha kula vyakula vikali, unaweza kuchagua chaguo lenye afya kama vile pilipili mbichi.

Send this to a friend