Vyanzo vikuu vinne vya ugonjwa wa Figo

0
66

Ugonjwa wa Figo huogopwa sana kwani sayansi ya matibabu haina tiba yake.

Magonjwa ya kudhoofisha ya figo yanaongezeka kwa haraka sana duniani kote. Wataalam wanasema mtu mmoja kati ya watu kumi ana aina fulani ya ugonjwa wa figo usiopona.

Mambo kadhaa kama kuongezeka kwa kisukari, matatizo ya shinikizo la damu, unene zaidi, uvutaji wa tumbaku na mafuta mengi mwilini (cholesterol) huchangia kupata ugonjwa wa figo.

Hivi ni vyanzo vikuu vya ugonjwa wa figo kwa mujibu wa tovuti ya Kidney Education.

Kisukari:
Kisukari ndicho sana sana husababisha ugonjwa wa figo. Asilimia 35- 40 ya magonjwa ya figo yasiyopona yote huletwa na kisukari. Tuseme kwa kila watu watatu walio na ugonjwa wa kisukari, mmoja wao anaweza kupata ugonjwa sugu wa figo.

Shinikizo la damu:
Hali hii isipotibiwa au isipodhibitiwa kwa njia inayofaa, huwa ni chanzo kikubwa cha ugonjwa wa figo. Asilimia 30 ya magonjwa ya figo yasiyopona huletwa na shinikizo la damu. Hata kama ugonjwa wa figo umesababishwa na hali nyingine, shinikizo la damu hudhuru figo zaidi.

Ugonjwa wa uvimbe kwenye figo (Glomerulonephritis)
Ugonjwa huu ni wa tatu katika kuchangia magonjwa yote yanayoleta magonjwa sugu ya figo.

Polycycystic Kidney Disease
Shida hii ya uvimbe kwenye figo zote mbili ni ugonjwa unaoweza kurithiwa (toka kwa wazazi). Hali hii husababisha ugonjwa wa figo kutokana na uvimbe (cysts) kwenye figo zote.

Sababu nyingine: Figo kuzeeka, kufunga kwa mishipa iendayo kwenye figo (renal artery stenosis), mkojo kuzuiwa na mawe ya figo au tezi dume iliyo karibu na kibofu kuvimba, figo kuharibiwa na dawa fulani, maambukizo ya figo ya mara kwa mara kwa watoto na pia kupunguka kwa ukubwa wa figo na mwisho mkojo kurudi nyuma.