Vyumba vya madarasa Sengerema vyageuzwa madanguro

0
83

Wananchi wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wamelalamikia baadhi ya vyumba vya madarasa wilayani humo kugeuzwa sehemu ya kufanyia ngono licha ya vyumba hivyo kutumika asubuhi na watoto kujifunzia.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Amina John amewatupia lawama walimu wakuu kushindwa kufanya ukarabati wa vyumba hivyo vinavyodaiwa kuchakaa na kukosa milango licha ya Serikali kupeleka fedha za ruzuku za ukarabati kwenye shule hizo.

Serikali kuchukua hatua video ya wanafunzi inayosambaa mitandaoni

Inadaiwa pia suala hilo lilijadiliwa katika kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya Sengerema kilichokaa Oktoba 28, mwaka huu huku kikitoa mwezi mmoja kwa halmashauri hiyo kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha za ruzuku.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Binuru Shekidele amekiri kuwepo kwa hali hiyo na kuahidi kuwa watakaobainika watachukuliwa hatua.

Naye Ofisa Elimu Msingi wa halmashauri hiyo, Donati Bunonozi amesema hakuna fedha ya ruzuku inayoliwa na kudai kuwa zinafanya ukarabati kulingana na mwongozo wa Serikali unavyosema.

Chanzo: Mwananchi