Vyuo 10 bora zaidi Kusini mwa Jangwa la Sahara mwaka 2023

0
13

Tanzania imekuwa nchi pekee kutoka Afrika Mashariki yenye vyuo vikuu viwili katika orodha ya vyuo vikuu 10 boa iliyotolewa na jarida la Times Higher Education linaloangazia vyuo vikuu vinavyofanya vizuri zaidi Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Takwimu hiyo imeandaliwa kwa lengo maalum la kutathmini athari ya vyuo vikuu katika kukabiliana na changamoto kubwa katika eneo hilo lenye watu zaidi ya bilioni 1.3 pamoja na kusaidia kujulikana kwa vyuo vikuu ambavyo ni muhimu kwa maendeleo ya kijamii.

Hii ni orodha ya vyuo vikuu bora zaidi Kusini mwa Jangwa la Sahara mwaka 2023;

1. University of the Witwatersrand – Afrika Kusini
2. University of Johannesburg – Afrika Kusini
3. Muhimbili University of Health and Allied Sciences – Tanzania
4. University of Pretoria – Afrika Kusini
5. Makerere University – Uganda
6. University of the Western Cape – Afrika Kusini
7. Covenant University – Nigeria
8. UGHE – University of Global Health Equity – Rwanda
9. Ashesi University – Ghana
10. Ardhi University – Tanzania

Aidha, baadhi ya wataalam wa elimu wanadai kuwa mchakato wa kupata vyuo vikuu bora haujawa wazi na wa kweli kupitia viwango hivyo.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Raphael Chibunda ambaye taasisi yake imekuwa miongoni mwa vyuo bora nchini na kupata hadhi ya kimataifa kupitia viwango vingine katika miaka ya hivi karibuni, amesema hawakuweza kushiriki katika orodha hiyo kutokana na taratibu zilizotumika.

“Hatukutuma maombi ya viwango hivyo kwa sababu wanadai malipo. Inaonekana kama biashara,” Prof. Chibunda amebainisha.

Amesema chuo cha SUA kinashiriki katika viwango vingine, kama vile webometrics (uorodheshaji wa vyuo vikuu), ambavyo vigezo vyake vinajulikana.

Naye, mshauri wa masuala ya elimu kutoka jijini Dar es Salaam, Dkt. Thomas Jabir amedai “Huu ni mkakati wa uuzaji/utangazaji unaolenga kuinua hadhi ya kimataifa ya taasisi zinazoshiriki. Kwa hiyo hatuwezi kusema kwamba wote walio kwenye orodha hiyo ni bora zaidi.”

Send this to a friend