Vyuo vikuu 10 bora Afrika Mashariki

0
135

Elimu ya juu barani Afrika inaendelea kukua kadri miaka inavyozidi kusonga tofauti na miaka ya nyuma. Vyuo vingi vimeendelea kuboreshwa huku vijana wengi wakipata nafasi ya kujiunga na vyuo vikuu.

UniRank imetoa orodha ya vyuo vikuu bora barani Afrika kulingana na vigezo vyao na sifa kama vile kuwa na leseni kutoka kwa mamlaka inayohusika na elimu ya juu katika kila nchi, kutoa shahada au uzamili na udaktari kwa muda wa angalau miaka mitatu, na kutoa programu zake kwa kiasi kikubwa katika mfumo wa ana kwa ana, na si elimu kwa njia ya mtandao.

UDSM na UDOM vyakabiliwa na upungufu mkubwa wa wakufunzi

Kwa ukanda wa Afrika Mashariki, hivi ni vyuo vikuu 10 bora;

  1. Chuo Kikuu cha Nairobi (Kenya): nafasi ya 7 Afrika
  2. Chuo Kikuu Makerere (Uganda): nafasi ya 16 Afrika
  3. Chuo Kikuu Kenyatta (Kenya): nafasi ya 28 Afrika
  4. Chuo Kikuu Strathmore (Kenya): nafasi ya 31 Afrika
  5. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Tanzania): nafasi ya 37 Afrika
  6. Chuo Kikuu Mount Kenya (Kenya): nafasi ya 54 Afrika
  7. Jomo Kenyatta Agriculture and Technology (Kenya): nafasi ya 57 Afrika
  8. Chuo Kikuu cha Rwanda (Rwanda): nafasi ya 62 Afrika
  9. Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani Afrika (Kenya): nafasi ya 66 Afrika
  10. Chuo Kikuu cha Egerton (Kenya): nafasi ya 71 Afrika