Vyuo vya IFM na TIA vyatakiwa kubuni vyanzo vipya vya mapato ya serikali

0
11

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhandisi Hamadi Yussuf Masauni, amekiagiza Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) kufanya tafiti zitakazo ibua vyanzo vipya vya mapato na kodi ili kuisaidia Serikali katika kutekeleza mipango ya maendeleo kwa Watanzania.

Mhandisi Masauni amesema kuwa vyuo hivyo vimekuwa vikifanya vizuri katika mambo ya taaluma kwa kuongeza kozi mbalimbali, idadi ya wanafunzi licha ya changamoto ya miundombinu na ufaulu lakini suala la utafiti linatakiwa pia kupewa msukumo wa ziada.

“Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2021/22 imepokelewa vizuri na wabunge na wananchi kwa ujumla hususani katika mabadiliko ya kodi na vyanzo vya mapato, lakini jambo hili linaweza kuwa endelevu kwa kufanya tafiti zaidi ili kuweza kuwa na kodi na vyanzo vipya vya mapato ambavyo si kero kwa mwananchi,’’ ameeleza Mhandisi Masauni.

Ametaka tafiti hizo kujikita katika eneo la ununuzi na ugavi na kutoa ushauri kwa Serikali ili kuongeza nguvu katika usimamizi wa fedha za miradi kwa kuwa fedha nyingi hutengwa kwa ajili ya maeneo hayo.

Send this to a friend