Waafrika 17 akiwemo Mtanzania waokolewa kwenye biashara ya ukahaba India

0
69

Polisi nchini India wamewaokoa wanawake 17 wanaotokea Afrika Mashariki kutoka katika biashara ya ukahaba katika wilaya ya Hyderabad baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

Kwa mujibu wa vyombo vya ndani vya India, kati ya wanawake hao 17, 14 ni Wakenya, wawili ni Waganda, na mmoja ni Mtanzania.

Kikosi cha Kupambana na Usafirishaji wa Binadamu cha polisi kilivamia nyumba moja huko Kondapur na kuwakamata washukiwa watatu wanaotuhumiwa kuendesha biashara hiyo haramu.

Baada ya kukagua nyumba hiyo, polisi walikamata pesa taslimu, simu nne za mkononi, seti 25 za vifaa vya kupima virusi vya UKIMWI, ‘sexy toys’, na mipira ya kondomu 104.

Chapisho hilo lilieleza kuwa kiongozi wa kundi hilo aliwashawishi wateja kupitia programu za mitandao ya kijamii na kuwasafirisha wanawake hao kwenda katika miji mbalimbali nchini India.

“Alianzisha sehemu kwenye tovuti ya matangazo ya ‘Locanto’ ambapo aliweka wasifu wa wanawake na kuendesha biashara yake ya ukahaba. Wanawake hao wamekuwa wakizunguka katika miji mbalimbali ikiwemo Delhi, Mumbai, Bengaluru na Hyderabad,” imeeleza taarifa ya polisi.

Inasemekana kuwa wanawake hao walifika India kwa kutumia visa za kitalii na matibabu lakini walibakia nchini humo baada ya visa zao kumalizika.

Send this to a friend