Waasi DRC watangaza kusitisha mapigano

0
6

Muungano wa waasi Mashariki mwa DRC unaojumuisha M23 umetangaza kusitisha mapigano kutokana na sababu za kibinadamu kuanzia Februari 4, mwaka huu.

Muungano huo umeongeza kuwa haukuwa na nia ya kuuteka Bukavu, Mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini, baada ya kuuteka mji mkubwa wa Goma wiki iliyopita.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zimesema takriban watu 900 wameuawa na wengine 2,880 kujeruhiwa katika mapigano DRC.

Rais wa Rwanda asema hajui kama wanajeshi wake wako DRC

Muungano wa makundi ya waasi unaojulikana kama Muungano wa Mto Congo umeshutumu Jeshi la Congo (Congo River Alliance) kwa kuua watu wakitumia ndege kupiga mabomu maeneo wanayoshikilia.

Hata hivyo, mataifa ya G7 na EU yamelaani mashambulio hayo kama ukiukaji wa wazi wa uhuru wa DR Congo.

Send this to a friend