Waathirika wa ajali ya Precision Air kulipwa TZS bilioni 396

0
63

Kamishna wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware amesema waathirika wa ajali ya ndege ya Precision Air watalipwa fidia zao haraka iwezekanavyo.

Akizungumza jijini Dodoma katika semina ya Wabunge kuhusu usalama barabarani, Dkt. Saqware amesema, ndege hiyo ilikuwa na bima halali ambapo ilikata kutoka wakala wa ndani na nje ya nchi.

Aidha, amesema fidia itakayolipwa kwa Shirika la Ndege la Precision ni zaidi ya dola milioni 50 za Kimarekani (sawa na TZS bilioni 116) na waathirika watalipwa zaidi ya dola za kimarekani milioni 170 (sawa na TZS bilioni 396).

Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa ameitaka Mamalaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kuharakisha ulipaji fidia kwa waathirika (waliofariki na walionusurika).

“Tunaomba TIRA nendeni mkasimamie bima iliyokatiwa katika shirika lile iweze kulipa watu wale wote, kwa maana waliofariki na walionusurika,” amesisitiza.

Jumla ya watu waliokuwa katika ajali hiyo ilitokea Novemba 06 mwaka huu katika Ziwa Victoria Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera ni 43, ambapo watu 19 walifariki dunia na 24 waliokolewa.

Send this to a friend