Waathirika wa corona Tanzania wafikia 170

0
46

Wizara ya Afya visiwani Zanzibar imetangaza ongezeko la wagonjwa wapya 23 wenye maambukizi ya virusi vya corona, hivyo kufanya idadi ya visa vilivyoripotiwa hadi sasa kufikia 58.

Kati ya wagonjwa hao wapya, wagonjwa 21 ni raia wa Tanzania, mmoja ni raia wa Ufaransa na mmoja ni raia wa Cuba ambao wote wanaishi visiwani humo.

Wagonjwa wawili kati ya wagonjwa hao wapya wamefariki wakiwa majumbani mwao kabla ya kuchukuliwa vipimo, hivyo kufanya idadi ya waliofariki kwa maambukizi ya COVID-19 kufikia watatu.

Serikali imeendelea kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa huo, huku ikiwahimiza wenye dalili kutoa taarifa mapema na kuepuka kujichanganya na watu wengine ili kudhibiti maambukizi.

Send this to a friend