Wabunge Kenya waomba ulinzi baada ya kuunga mkono kuondolewa kwa Gachagua

0
80

Wabunge nchini Kenya wametaka kuhakikishiwa usalama wao kufuatia kuwasilishwa kwa hoja ya kumtimua Naibu Rais wa nchi hiyo, Rigathi Gachagua.

Mmoja wa wabunge hao, Junet Jumanne amemtaka Spika Moses Wetangula kuwasiliana na Inspekta Jenerali wa Polisi aliyeteuliwa hivi majuzi, Douglas Kanja ili kuwahakikishia usalama wabunge 291 waliopiga kura kuunga mkono hoja ya kuondolewa madarakani.

Mbunge huyo mwenye msimamo mkali , amedai kwamba baadhi ya wabunge walionyesha hofu kuhusu kuunga mkono hoja hiyo kwa sababu unahusisha kumondoa Naibu Rais, ambaye ni kiongozi wa pili wa juu serikalini.

“Tumemkabidhi Inspekta Jenerali wa Polisi, Bwana Kanja, kuhakikisha usalama wa wabunge 291. Kile tunachofanya si jambo dogo; wakati Trump aliondolewa nchini Marekani, tulijua kile kilichokuwa kinafanyika. Tusiwe na chuki kwa yeyote kwa sababu hii inafanywa Kikatiba. Wakati wabunge walipokuwa wakisaini, waliniambia; tunaunga mkono lakini tunataka mambo yafanyike kwa sheria ndani na nje ya bunge,” amesema.

Wabunge wengi wanamtuhumu Gachagua kwa kugawanya Wakenya kwa misingi ya kikabila, kuhujumu urais, kukiuka kiapo cha ofisi na kukinzana na Sheria ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa, kudaiwa kujilimbikizia mali ya Ksh.5.2 bilioni [TZS trilioni 14.15] kupitia njia za ufisadi, kuchochea umma dhidi ya maagizo ya serikali ya Kaunti ya Nairobi, utovu wa nidhamu na uonevu.

Send this to a friend