Wabunge wa upinzani watakiwa kwenda bungeni na fomu zinazoonesha hawana corona

0
32

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewataka wabunge wa upinzani
waliotii amri ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kutohudhuria vikao vyya bunge kurejesha posho walizolipwa.

Spika Ndugai amesema hilo leo Mei 6, 2020 bungeni mjini Dodoma ambapo ameongeza kuwa wakati wabunge hao walipoadhimia kutohudhuria vikao vya bunge kwa muda wa wiki mbili, tayari walikuwa wamelipwa posho za vikao zaidi ya TZS 2 milioni kila mmoja.

Aidha, amewataka wabunge hao watakapoamua tena kwenda bungeni wawe na fomu
za daktari zinazothibitisha kuwa hawana maambukizi ya virusi vya corona.

Maagizo hayo yametolewa kufuati baadhi ya wabunge wa vyama vya upinzani kuadhimia kutohudhuria vikao vya bunge, kwa maelezo kuwa wapo karantini wakifuatilia afya za hali zao kama wana maambukizi ya virusi hivyo ama la.

Send this to a friend