Wachezaji wa Simba, Yanga na Singida hatarini kuzuiliwa Ngao ya Jamii

0
90

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema mpaka sasa ni Azam FC pekee iliyowasilisha vibali 10 vya wachezaji wa kigeni ambao wanastahili kucheza kwenye michezo ya Ngao ya Jamii, mkoani Tanga.

TFF imesema hakuna mchezaji yeyote kutoka Singida Fountain Gate, Simba SC na Young Africans ambaye ataruhusiwa kucheza mashindano hayo kama hatakamilisha taratibu za kisheria.

Uwanja wa Mkapa wafungwa hadi Oktoba 20

Mashindano ya Ngao ya Jamii yanatarajia kuanza leo Agosti 09, 2023 ambapo Yanga SC itafungua dimba kwa kuzichapa na Azam FC saa moja jioni.