Wachimbaji wadogo Wisolele kupata umeme ifikapo Oktoba

0
45

Waziri wa Nishati, January Makamba ameahidi kupeleka umeme kwenye migodi ya wachimbaji wadogo katika Kijiji cha Wisolele ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu ikiwa ni moja ya vipaumbele vya Wizara kupeleka umeme kwenye maeneo ya uzalishaji, ikiwemo migodi.

Makamba aliitoa ahadi hiyo jana wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga baada ya kufika katika eneo hilo na kujionea shughuli za uchimbaji na uchenjuaji madini ambapo wachimbaji walilalamika kutumia gharama kubwa kuendesha mitambo kwa kutumia mafuta.

“Serikali baada ya kujua mahitaji ya umeme katika maeneo kama haya tukaweka mpango wa kuleta umeme kwenye maeneo ya uzalishaji ikiwamo migodi na Wisolele. Mpango wa manunuzi upo hatua ya mwisho na tunatarajia mwisho wa mwezi huu tutamtangaza mkandarasi atakayeleta umeme hapa,” amesema Makamba.

Katibu Mkuu Mstaafu apinga kuandikwa katiba mpya

Aidha, amesema Serikali imetenga shilingi milioni 336 kupeleka umeme kwenye eneo hilo hivyo ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu kazi ya uwekaji miundombinu ya umeme itakuwa imeshaanza.

Ili kuwasogezea huduma wachimbaji hao, amesema TANESCO imeanzisha mfumo wa viunga vya huduma ambapo maeneo yenye watu wengi wanaweka gari pamoja na watumishi kwa masaa 24 ili zinapotokea changamoto iwe rahisi kuwahudumia wananchi ndani ya muda mfupi, na Wisolele ni moja ya viunga hivyo.

Katika hatua nyingine, Makamba amewaagiza TANESCO kuhakikisha kuwa ndani ya wiki mbili wanaunganisha umeme kwa wateja wote walioomba kuunganishiwa huduma hiyo katika Kata ya Kagongwa wilayani Kahama, baada ya wananchi wa eneo hilo kulalamikakucheleweshewa kuunganishiwa umeme licha ya hatua za maombi kukamilika.

Send this to a friend