Wachungaji 17 wa KKKT wafukuzwa kazi kwa uasi

0
24

Katika hali isiyo ya kawaida wachungaji 17 wa Kanisa la Kanisa la Kinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde wamefukuzwa kazi tuhuma za kukiuka maadili ya kikristo na wito wa kazi hiyo.

Katibu mkuu wa dayosisi hiyo, Mchungaji Ikupilika Mwakisimba amesema wachungaji hao wamekuwa wakipinga kuhamishwa makao makuu ya dayosisi kutoka Tukuyu wilayani Rungwe kwenda jijini Mbeya.

Mwakisimba anasema wachungaji hao walitangaza uasi kwa kukataa maelekezo ya Askofu wa KKKT Dayosisi ya Konde, Dkt. Edward Mwaikali pamoja na kuandika waraka wa kutokuwa na imani na halmashauri kuu ya dayosisi hiyo.

“Baadhi ya wachungaji kutoa waraka na matamko ya kutokuwa na imani na askofu na halmashauri kuu kuna maana ya kuikana ajira yao, yaani, gross insurbodination [kuidharau/kutoitii mamlaka],” amesema Mwaikali.

Licha ya matendo yao Mwaikali amesema uongozi kanisa ulijaribu kuwaonya wachungaji hao na kuwasihi wasichanganye mambo ajira, hisia na itikadi za kisiasa lakini walishupaza shingo.

Send this to a friend