Wadaiwa kuiba gari la wagonjwa na kulifanya la watalii Mara

0
23

Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia watu wanne kwa tuhuma za kuiba gari la wagonjwa (Toyota Land Cruiser) lililokuwa likitoa huduma katika Hospitali ya Manispaa ya Musoma kisha kulibadilisha kuwa gari la biashara ya kubeba watalii.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoani humo imesema kufuatia kupokelewa taarifa hizo, Jeshi la Polisi lilianza mara moja uchunguzi na ufuatiliaji wa kina, hatua iliyowezesha kubaini namna gari hilo lilivyotolewa pamoja na eneo lilipokuwa limefichwa.

Polisi wamesema gari hilo liliibwa Oktoba 25, 2025 likiwa kwenye eneo la maegesho ya hospitali, na baada ya ufuatiliaji, lilipatikana likiwa kwenye hatua za mwisho za kubadilishwa mwonekano.

Send this to a friend