Wadukuzi warusha picha za utupu kwenye mkutano wa Spika wa Bunge la Afrika Kusini

0
74

Katika kupambana na virusi vya corona, shughuli mbalimbali zinazohusisha mikusanyiko ya watu kama vile mikutano zimezuiwa katika nchi mbalimbali, huku watu wakishauriwa kufanya mikutano hiyo kwa njia ya video.

Licha ya kamati ya bunge la Afrika Kusini kuitikia wito huo na kufanya mkutano kwa njia ya video, mambo hayakwenda kama yalivyopangwa.

Mapema leo asubuhi wakati kikao kikiendelea, udukuzi ulifanyika na picha za utupu za watu zikaonekana kwenye kioo, huku sauti ya mwanaume ikimtusi Spika wa Bunge, Thandi Modise aliyekuwa anaongoza kikao hicho.

Wabunge waliokuwa kwenye kikao hicho wamesema kitendo hicho ni cha kufedhehesha na chenye kukera sana.

Baada ya muda wataalamu wa bunge walitengeneza kiungio (link) kipya ambapo wabunge waliweza kujiunga na kuendelea na kikao.

Send this to a friend