
Wadukuzi nchini India wamedukua video za CCTV Camera katika moja ya hospitali ya uzazi nchini humo zinazoonesha baadhi ya wajawazito wakipatiwa matibabu, kisha kuziuza kwenye mitandao ya kijamii.
Polisi nchini India wamesema hakuna mwanamke yeyote aliyewasilisha malalamiko dhidi ya tukio hilo.
Akizungumza na BBC, Mkurugenzi wa hospitali hiyo amesema kuwa kamera hizo zimewekwa kwa ajili ya usalama wa madaktari.







