Wahadzabe wapewa nyama ya Nyumbu 20 ili wakubali kuhesabiwa

0
85

Jamii ya wahadzabe iliyopo katika eneo la Yaeda, Mkoa wa Manyara wamekabidhiwa kitoweo cha nyama pori aina ya Nyumbu na Mkuu wa Mkoa, Makongoro Nyerere ikiwa ni takwa la jamii hiyo kupewa kitoweo hicho ili kushiriki Sensa ya Watu na Makazi leo Agosti 23.

Kiongozi wa Kimila wa jamii ya Hadzabe, Athuman Mangula amesema awali takwa la jamii hiyo lilikuwa ni kupewa kitoweo cha mbuni na Serikali, na badala yake wamepewa nyumbu huku akieleza kuwa manyoya ya mbuni hutumika kama tiba endapo wakipata ugonjwa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere amesema ombi hilo limepokelewa na litafanyiwa kazi, huku jumla ya nyumbu 20 zikitolewa bure na Serikali kwa jamii hiyo.