Tanzania Bara leo imeadhimisha kutimiza miaka 60 tangu bendera ya mkoloni Mwingereza iliposhushwa na ile ya Tanganyika kupandishwa na hivyo kuwa nchi huru.
Kupata uhuru kwa Tanganyika kulifanya Mwalimu Julius Nyerere kuwa Waziri Mkuu wa kwanza, lakini mwaka 1962 Tanganyika ilikuwa Jamhuri na Mwl. Nyerere kuwa Rais wa kwanza.
Katika mapamabano ya kumwondoa mkoloni, Mwalimu Nyerere hakuwa peke yake, bali alikuwa na wenzake 16 ambao ndio walikuwa mstari wa mbele, huku wakiungwa mkono na wananchi.
Mbali na Mwalimu, wengine ni;
1. Abuu Sykes
2. Aboubark Lilanga
3. Ally Sykes
4. Cathbert Oswald Milinga
5. Dosa Aziz
6. Jamanus Pacha
7. Japhet Kirilo
8. John Rupia
9. Joseph Kamalando
10. Joseph Kaselabantu
11. Kisunguta Gabara
12. Lameck Makaranga
13. Patrick Kunambi
14. Sadan Abdul Kandoro
15. Suleiman Kitwara
16. Tewa Said Tewa
Wengi wa waasisi wa uhuru wa Tanganyika wamefariki, na akilihutubia Taifa Rais Samia Suluhu Hassan Desemba 8, 2021 alisema kwamba ingekuwa furaha endapo waasisi hao wangekuwepo kuona matunda ya juhudi zao.
Tanganyika iliungana na Zanzibar mwaka 1964 na kuunda Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ambayo inadumu hadi leo.