Wafanyabiashara wa vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki watakiwa kuomba leseni TCRA

0
40

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka watu wote wanaofanya biashara ya uingizaji, usambazaji na uuzaji wa vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki kuwa na leseni kutoka mamlaka hiyo yenye dhamana ya kusimamia sekta ya mawasiliano nchini.

TCRA imeeleza kuwa kwa mujibu wa Sheria ha Mawasiliano ya Kielektroniki ya mwaka 2010 (EPOCA 2010), kila muingizaji, msambazaji na muuzaji sa vifaa vya mawasiliano ya kielektroniki anatakiwa kuwa na leseni ya kufanya shughuli hiyo, na kwamba kutokuwa nayo adhabu ni faini isiyopungua TZS milioni 5  au kifungo cha muda usiopungua miezi 12 au vyote kwa pamoja.

Kwa mujibu wa taarifa ya mamlaka hiyo ya Oktoba 26, 2020, wafanyabiashara hao wametakiwa kuomba leseni ndani ya siku 30 kwa kupeleka maombi ambayo hufanyika kwa njia tovuti ya TCRA, www.tcra.go.tz, na kulipa gharama stahiki.

Mamlaka hiyo imesema watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo ndani ya muda tajwa watafungiwa biashara zao na kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria.

Send this to a friend