Wafanyakazi Ufaransa wagoma, waandamana kupinga kuongezwa umri wa kustaafu

0
30

Vyama vya wafanyakazi nchini Ufaransa vimeshiriki mgomo wa kitaifa ikiwemo kufanya maandamano ya kupinga mpango wa serikali ya nchi hiyo wa kuongeza umri wa kustaafu kwa wafanyakazi.

Maandamano hayo yamefanyika katika miji mikuu ya Ufaransa ikiwa ni pamoja na Paris, Marseille, Toulouse, Nantes na Nice ambayo imepelekea huduma za usafiri kusimama, shule za msingi kufungwa pamoja na Mnara wa Eiffel kufungwa.

Vyama vya wafanyakazi vimeanzisha maandamano hayo dhidi ya mabadiliko ya pensheni yaliyotolewa na serikali ya Rais Emmanuel Macron ambapo sheria itawahitaji raia wa Ufaransa kufanya kazi hadi miaka 64 kutoka 62 iliyopo, ili kupata pensheni kamili ya serikali.

Upinzani Afrika Kusini kuishtaki Serikali kutokana na kukatika kwa umeme

Kulingana na Wizara ya Elimu ya Ufaransa, zaidi ya asilimia 40 ya walimu wa shule za msingi na zaidi ya theluthi moja ya walimu wa shule za sekondari wako kwenye mgomo huo.

Kwa mujibu wa CNN, mapendekezo hayo yamekuja wakati ambao wafanyakazi nchini Ufaransa wanadai mishahara kutokidhi gharama za maisha pamoja na mazingira yasiyoridhidha ya kazi.

Send this to a friend