Wafanyakazi wa Kenya Pipeline kwenda jela kwa wizi wa mafuta

0
13

Wafanyakazi wawili wa zamani wa Kampuni ya Kenya Pipeline (KPC) wamehukumiwa kulipa faini ya Ksh milioni 10 kila mmoja [TZS milioni 202.06] au kutumikia kifungo cha miaka 9 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa ya wizi wa mafuta ya petroli na kuingilia mifumo ya KPC kinyume cha sheria.

Waliopatikana na hatia ni Reuben Andolo Aseneka, aliyekuwa mfanyakazi wa kituo cha kupakia mafuta, na Mutai Micah, aliyekuwa mfanyakazi wa ICT kwenye kampuni hiyo.

Wawili hao wamehukumiwa pamoja na Joseph Mbugua Maina, dereva wa lori ambaye amehukumiwa kulipa faini ya Ksh. milioni 5.3 [TZS milioni 107.09] au kutumikia kifungo cha miaka 7 jela.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkuu wa mahakama ya Kisumu, D.O. Onyango amesema kuwa uhalifu wa mafuta unapaswa kukomeshwa na hukumu hiyo iwe funzo kwa wale wanaopanga kutenda makosa kama haya.

Hukumu hiyo inakuja wakati ambapo serikali ya Kenya inazidi kuimarisha udhibiti wa rasilimali zake ili kuhakikisha mafuta hayapotei kupitia njama za kihalifu.

Send this to a friend